Sunday, 23 September 2018

UVIMBE KWENYE KIZAZI. FIBROID


Imeandikwa na dr.Ibu


Mazoea ni kwamba mtu akisema kizazi anamaanisha uterus..

Hii ndio mara kwa mara mnasikia mkipigwa utrasound huko wanakuambia una uvimbe kwenye kizazi. Watu wengi wakasema nizungumzie.

Sasa huu ni moja ya aina ya uvimbe ambao unakuwa kwenye kuta za kizazi/Uterus. Ni uvimbe ambao ndio unaongoza kati ya aina zote za uvimbe kwenye kuta za kizazi. Mungu mkubwa uvimbe huu sio kansa na uwezekano wa kuwa kansa ni mdogo sana ni chini ya 0.1% maana yake ni mtu mmoja kati ya watu wenye uvimbe 1000.

Inakadiriwa kwamba 20% ya wanawake wakifika umri wa miaka 30 basi wanakuwa wameshapata fibroid. Uzuri ni kuwa asilimia kubwa 50% huwa hawana dalili yoyote wako freshi tu na hauwasumbui hata kidogo.
Na uvimbe huu huwapata zaidi watu :

1.weusi kuliko wenzetu wa rangi nyeupe.
2.watu ambao hawana watoto au wenye ugumba wa mtoto mmoja. Maana yake ana mtoto mmoja lakini anajaribu kupata ujauzito tena hawapati.

3.umri ambao wanakuwa wengi wanapata ugonjwa huu ni miaka kati yaa 35 na 45.
4.urithi kifamilia kama kuna mtu ana uvimbe na wanawake wengine kwenye familia kuna uwezekano wa kuwa na uvimbe japo sio lazima.

Ukuaji wa uvimbe huu hutegemea homoni ya estrogeni.. ndio maana

1.Huwa unaongezeka kwa watu ambao bado wanaona siku zao wakishaacha kwenye miaka ya 50 unapungua na baadae unaweza kupotea kwa sababu estrogen inakuwa imepungua sana mwilini

2.unaongezeka zaidi kipindi cha ujauzito kwa sababu homoni inakuwa nyingi kwenye mwili.

3.Haiwezi kutokea kabla ya kubalehe/ Kuvunja ungo kwa sababu homoni pia zinakuwa kidogo.

4. Baada ya kuacha siku zake mwanamke hawezi kuota fibroid mpya na zilizokuwepo zinapungua au kupotea kabisa kwa kunyauka.

5.inawapata watu wanene zaidi kwa sababu mafuta huwa yanaweza kutengeneza hizo homoni kwenye mwili.
6. Watu wanaotumia dawa za uzazi wa mpango zenye homoni moja.Ila hizo ambazo mnatumia sana siku hizi hazina uhusiano na fibroid.

Fibroid inaweza ikawa moja au zaidi ya moja na ukuaji wake huwa hauwi sawa nyingine inaweza kukua haraka kuliko nyingine.

Uvimbe huu chanzo chake kamili hakijulikani kisayansi.  Lakini kuna mawazo ya wanasayansi wengi wakisema unatokana na misuli ya kuta za uzazi kubadilika na kukua haraka zaidi ya kawaida na mwili kushindwa kuukontrol..
 Kwa hiyo mgonjwa anakuja hospital anaweza kuwa na mtoto mmoja mkubwa kuanzia miaka 10 nakuendela au hana mtoto kabisa...
Japo wakati mwingine wengine wanaweza wakawa na watoto wengi lakink kama amezaa akiwa na umri mdogo na akazaa mara kwa mara anaweza akawa kwenye kundi hili hatarishi kupata fibroid...umri wa kati ya miaka 35 hadi 45.

Dalili za  fibroid
Kama nilivosema zaidi ya 75% hazina dalili basi hugundulika kwa bahati tu kama hivo ukipiga utrasound au dr akiwa anagusa tumbo akaona kuna uvimbe.
Lakini kama dalili mara nyingi hutegemeana na ukubwa na sehemu ilipo.

1.kutoka damu nyingi ya hedhina inayoendelea kuzidi kila mzunguko. Hii ni kwa sababu inazuia kujiminya kwa mishipa ya damu ya kwenye kuta za kizazi ili damu isitoke.

2.mzunguko kuwa hautabiliki...kwenda hedhi mara nyingi zaidi ya kawaida.

3.maumivu wakati wa hedhi
4.maumivu wakati wa tendo
5.kushindwa kupata mimba
6.kupoteza mimba mara kwa mara kwasababu nafasi imejaa uvimbe kwahiyo mimba zinatoka
7.tumbo kuuma chini ya kitovu
8.kuvimba chini ya kitovu



Mchoro kuonesha aina mbalimbali za fiboid kutokana na eneo zilipo




Wednesday, 19 September 2018

SWALI:Doctor samahani naomba kuuliza swali. ninapokuwa natoa haja kubwa mgongo/kinyama kinatoka,sipati mauivu yoyote ila lazima nikirudishe kwa kidole naomba kujua nini hiki na kama kina athari kiafya

JIBU
Ugonjwa wako unaitwa bawasiri
Bawasili au hemorrhoids kitaalamu

Ni ugonjwa ambao hutokana na kuvimba kwa mishipa ya damu ambayo ipo sehemu ya chini ya njia ya haja kubwa(mkundu)

 Mishipa hii huvimba taaratibu na damu yake huweza aidha kuganda( thrombosed) au kuathiriwa na wadudu ( infected) na hapo ndio huwa na maumivu lakini la sivyo huwa haiumi.

Bawasiri zimegawanyika makundi mawili zipo ambazo hukaa ndani kabisa (internal hemorrhoids) na nyingine huwa zinakuwa nje na kwa juu zinakuwa zimevikwa ngozi ya kawaida pale kwenye mlango wa kuingilia (external hemorrhoids )...

NINI HUSABABISHA.
sababu kubwa ya kupata bawasiri ni hali ya wima ya binadamu tuliyonayo ambayo inasababisha damu inayoenda eneo la chini ya mwili kama miguu kutokana kushindwa kupanda juu kirahisi hii ndio sababu wanyama kama mbuzi, mbwa ambao hawapo wima hawapati hemorrhoids, damu isipopanda haraka inasababisha mishipa ile kutanuka na kuvimba na ndio tunaita hemorrhoids.

2. Kupata choo kikavu/ kigumu sana kutokana na kutokunya maji ya kutosha na vyakula vyenye nyuzi kama mboga za majani na matunda. Hii husababisha kubanwa kwa mishipa ya damu na kuzuia damu kupanda juu kurudi kwenye moyo na hivyo huleta uvimbe...

3. Kuwa na pressure kubwa tumboni...

Hii huzuia pia damu kurudi juu kwenda kwenye moyo kirahisi..hii huwapata watu  wenye uvimbe tumboni, au wajawazito, wanaofanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito na hao wenye constipation( choo kigumu) pia wazee wenye tezi dume au kansa ya kibovu cha mkojo

Zipo sababu nyingi lakini hizo ndio ambazo ni muhimu sana kwenu.


Dalili zake .
1. Kuhisi kuna kitu kipo ndani ya sehemu ya haja kubwa ambacho hakitoki
 Hisia hii huwa inategemeana na ukubwa wa uvimbe.
2. Huweza kutoka damu wakati wa kutoa haja kubwa
3. Maumivu wakati wa kutoa haja kubwa.
4. Kuhisi kuna kitu kinatoka na kurudi wakati wa kutoa haja kubwa.
5.kuona kabisa uvimbe umetokezea kwenye njia ya haja kubwa.

NB:uvimbe unaweza ukawa mmoja au zaidi ya mmoja. Mara nyingi hukaa sehemu kama ni saa ni sehemu ya saa 4, 7 na 11.

GRADE ZAKE..
1. Kunakuwa na uvimbe mdogo kwa ndani
2.uvimbe unakuwa unaweza kutoka nje mtu akijikamua tumbo na kurudi wenyewe akiacha kujikamua
3.uvimbe unakuwa unatoka mtu akijikamua na unaweza kurudishwa kwa kitu choxhote kama kidole na ikawezekana kukaa ndani

Grade 4. Unakuwa umetoka nje na hauwezi hata kurudishika ndani

MATIBABU NA NJIA ZA KUJIKINGA
 Matibabu yanategemeana na grade ya bawasiri.

Grade 1. Kuna dawa ambayo huwa tunachoma ambayo inakausha kabisa
Grade 2. Kuna ruber band wanaifunga kwa sehemu inapoanzia uvimbe(shina lake) alafu uvimbe wote unakauka kwa sababu unakosa damu

Au kuna kifaa kinaitwa stapler kinatumika kukata bawasiri mojamoja.

Grade 4 tunafanya operation  na kuna aina nyingi za operation.

Namna ya kujikinga.

1.kunywa maji ya kutosha
2.kula vyakula vya nyuzi nyuzi
3. Acha kunyanyua vyuma fanya mazoezi ya kawaida
4.fanya mazoezi kupunguza mwili
5. Usikae sana chooni.. kupokea simu au kusoma gazeti au kuchati chooni

6.tibu haraka kama una choo kigumu

7. Acha kujikamua wakati wa kukojoa au kutoa haja kubwa.

8. Ukijisikia haja kubwa usiibane nenda.
By @dr.ibu

SWALI:Nina shida naomba unisaidie..... Nilikua mjamzito early pregnancy ila jumatatu iliyopita nilifanya kaz ngumu ucku wake nkatokwa na dam nying sana nlienda hospital nkaambiwa mimba imetoka nlioshwa nkapewa dawa pamoja na sindano.... Dam ilikata kwa mda ila juz nliumwa sana na kutokwa na dam upya ila ikakata leo hali ileile imenirudia naomba nisaidie



 JIBU: Pole sana mom/dada... damu haitakiwi kuendelea kutoka ukiwa umeshasafishwa... uwezekano ni vitu viwili ni aidha  ilibakia hawakumaliza kitu ambacho uwezekano ni mdogo kama ikifanyika hospitali au kuna ugonjwa unaitwa   GTD (  Gestational Trophobastic Disease) ambao unaendelea kuwa na dalili za ujauzito hata kama mimba imeshatoka. Na ukipima mkojo kipimo cha mimba kinakuwa positive.   Kawaida mimba ikishatoka baada ya siku 14 kipimo cha ujauzito kile cha mkojo kinatakiwa kuwa negative lakini kwa hawa bado kinakuwa positive..


Chakufanya nakushauri nenda hospitali ya karibu kubwa ya wilaya, au mkoa au rufaa kaonane na daktari.. Utapigwa utrasound ambayo itaonesha vyote kama bado kuna mabaki ya mimba au huo ugonjwa wa GTD na pia utaangaliwa kama una upungufu wa damu na kama umepata maambukizi (infection) yoyote kwa kupima damu yako.  Alafu baada ya siku 14 kuisha unaweza kupima kipimo cha ujauzito kama nilivoeleza pale juu.  Pole sana mungu akusimamie upone. Alafu pia mimba ikitoka ni rahisi sana kupata mimba nyingine haraka sana kwa hiyo tunashauri watumie njia za uzazi wa mpango... na njia nzuri kwao ni loop ambayo unaweza kutoa na ukapata mimba muda wowote bila kusubiri kama sindano




Tuesday, 18 September 2018

SWALI: Doctor samahani naomba kuuliza swali, nina mtoto binti wa shule nimemkuta na miso chumbani kwake je dawa hiyo ina kazi gani?

Miso kama jina maarufu ndugu alivouliza hiko ni kifupi tu ila inaitwa misoprostol...ni dawa inayotumika zaidi kuongeza contraction ( kujikunja kwa kuta za  mji wa uzazi) na ndio maana wengine wanazitumia katika kutoa mimba... pia hospital tunatumia kusafishia kizazi au kutoa mimba ambayo imefia tumboni... pia tunaitumia kuzuia damu kutoka kama mama katoa damu nyingi sana baada ya kujifungua na hayo yote yana dose tofauti... kuna namna tofauti na maarufu ni ile ya kuweka kwenye kuta za uke lakini ipo ya kumeza pia.

Ushauri ni kwamba ni kwamba kapime kama wanao ni mjamzito basi anawweza akawa alikuwa anataka kuitoa mimba. Pia ongea nae taratibu madhara  ya kutoa mimba na  kutumia dawa bila kuandikiwa na daktari


Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri

kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo  https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU


Be healthy and happy

Dr.ibu

SWALI:Doctor samahan mama angu anatatizo limesumbua kwa mrefu , anadai kila akila chakula na akinywa maji, maji hayo yanaenda kubana sehemu ya juu upande wa kushoto na wa tumbo mauvivu makali sana anayapata. tatizo lake ni nini?


 Ila nadhani anacho maanisha ni kwamba akila chakula anapata maumivu yanayokuwa makali yanakuwa kama yanaunguza na yanazunguka mgongoni pande zote .

Hii ni aina ya maumivu yanayotokana na vidonda vya tumbo...

Watu kama hawa huwa inafika kipindi hawagusi chakula kabisa kwa sababu ya maumivu...aina hii ya vidonda vinakuwa kwenye mfuko wa tumbo kabisa ( stomach ulcer). Hawa huwa wanakonda sana kutokana na kuacha kula sababu ya maumivu


Aina nyingine ya vidonda vya tumbo( PUD) hizi hukaa kwenye utumbo mdogo (duodenal ulcer) hizi huuma wakati wa njaa hivyo watu kama hawa huwa hawavumilii njaa. Wakati mwingine wanaamka kabisa usiku kutafuta chakula au kupika hata saa nane usiku wanakula sana na wananenepa kupindukia.

Dawa zao ni zilezile dawa tatu  antibiotic mbili na moja kwa ajili ya kuzuia asidi amoxicillin pantoprazole na metronidazole anakunywa kwa siku 14 au ananunua kuna package  ipo na zote inaitwa heligokit.



Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri

kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo  https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU


Be healthy and happy

Dr.ibu





Monday, 17 September 2018

SWALI .Dr habar,samahan mm ni mjamzto wa miez mi3 sasa lakn pia nilianza bleed tarh 6 nkamalza tarh8 nkaenda kukutana na mpnz wa tarh 12-21ndpo nkaondoka jion lakn baada ya kuondoka skuondoka nilienda tena kukutana na mchepuko wang tarh 22 usku alikuwa anatoa nje pia nkakutana naye tena tarh 28 usku.mzunguko wangu ni a siku 28. plz naomba kujua hii mmba itakuwa ya yule wa kwanza au wapl plz naomba nijbu

JIBU
kwanza kabisa pole kwa msongo mawazo ambao upo nao kwa sasa.

Ukitaka kujua baba a mtoto unataakiwa kujua siku zako za hatari za kutungishwa mimba katika mzunguko wako. Katika mzunguko wa kila mwanamke kuna sehemu mbili(2 phases).

Sehemu ya folicular ambayo ni sehemu ambapo yai linapitia mabadiliko mbalimbali ili liweze kurutubishwa. Katika hatua hii pia kunakuwa na maandalizi ya kuta za mji a uzazi (uterus) ka ajili ya mimba kutunga na kutunzwa kwa miezi tisa (wiki 36 hadi 40). Phase a folicular haina idadi kamili ya siku ila huanza siku ya kwanza mwanamke anapoanza mzunguko wake (siku ya kwanza ya hedhi) hadi siku yai linapotoka kwenye ovari (ovulation day). siku hii hutofautiana kutokana na urefu wa mzunguko wa mwanamke husika.

sehemu ya luteal
Au kitaalamu luteal phase hii huwa ni sawa  kwa kila mwanamke. ni idadi a siku ambazo yai linaweza kuishi, hii huchukua siku 14 tu.

Kitu kingine cha msingi kujua ni kwamba mbegu ya kiume huweza kuishi kwa siku 2-3 (masaa 48-72) hivyo ukijamiiana siku tatu kabla ya yai kutoka litaikuta mbegu ya kiume na kuna uwezekano wa kurutubishwa na ukapata mimba.
Pia yai likishatoka kwenye ovari hukaa siku mbili mpaka tatu ndio hapo ukuta wake hua mgumu na mbegu haiwezi kutoboa ili kurutubisha. kwahiyo mtu akifanya mapenzi ndani ya muda huo ndio urutubishwaji hutokea


Mzunguko wa mwanamke unatofautiana ila wa kawaida ni kuanzia siku 21 hadi 35 hivyo basi hata siku zao za yai kutoka zinatofautiana isipokuwa tu luteal phase ambayo ni siku 14 hazibadiliki

ukitaka kujua siku ya yai kutoka unachukua idadi ya siku katika mzunguko unatoa 14 abazzo ni siku ambazo yai linaweza kuishi.

kwa swali la dada itakua 32-14 itakuwa 18. Kwahiyo siku yake ya yai kutoka inakuwa siku ya 18, ukiangalia tarehe tokea tarehe 6 siku 18 ni tarehe 23.  kumbuka yai linakaa siku tatu na shahawa zinakaa siku 3 kwa hiyo kila aliyefanya naye mapenzi siku tatu nyuma au mbele ya tarehe 23 ni muhusika.Kwahiyo kuanzia wa tarehe 20 hadi 26 wote wamo katika siku hatari.

Boyfriend alikuwa naye tarehe 20 na tarehe 21 ni siku hatari na akachepuka tarehe 22 ambayo ni siku hatari zaidi.

Lakini ukitumia sayansi kwamba jinsi siku zinavozidi kwenda mbegu ya kiume hua inazidi kupoteza nguvu wa tarehe 22 anakuwa na uwezekano mkubwa zaidi kwa sababu mbegu zake zilikaa siku moja tu ndio yai likafika.

Hata ukiongeza na kwamba alikua anamwaga nje bado yeye ndio kuna uwezekano kubwa zaidi kwa sababu njia hii huwa sio effective sana. uwezekano wake wa kuzuia ujauzito ni chini ya 30%

Jibu kamili ni DNA.

Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri

kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo  https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU


Be healthy and happy

Dr.ibu






Swali: Kuna dawa za kuzuia mimba zinaitwa P2 je hizo dawa ukiwa unatumia Mara kwa Mara huwa zina madhara yeyote kwenye mwili


JIBU:

P2 ni jina limezoeleka la dawa za kuzuia ujauzito kama mtu kafanya mapenzi katika siku za hatari.... ni njia ambayo inatumika sana lakini watu wengi hawaulizi matumizi yake au wanapuuzia matumizi kadri yanavotakiwa ...

Ukweli ni kuwa p2 ni dawa ambayo inatengezwa na hormone. Na inafanya kazi kwa kuchelewesha yai lisitoke kwenye ovari au kuzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye mji wa uzazi zipate taabu kusafiri kwa kuzalisha uteute mgumu utakaoipa shida shawahawa kusafiri na kurutubisha yai..

UNAMEZAJE??
ukiona umefanya mapenzi na ukahisi umefanya siku za hatari na hujapanga kupata mimba unatakiwa kumeza dawa hizo...dose ni vidonge viwili 150gm jumla ni either kumeza vyote viwili au unameza kimoja alafu unasubiri masaa 12 unameza kilichobaki au kumeza vyote viwili kwa pamoja.. ila ya kumeza vyote viwili ndio ina faida kubwa zaidi.

Lini unatakiwa kumeza dawa hizi?...

The earlier the better wazungu wanasema wazungu.. dawa hizi zinakukinga mpaka kwa muda wa masaa 72 siku tatu. Unaruhusiwa kutumia ndani ya masaa 72 baada ya kufanya sex... baada ya hapo hazikusaidii.. ila uwezo wa kuzuia mimba unapungua jinsi siku zinavyozidi kusogea mbele mfano ukinywa kidonge cha kwanza ndani ha masaa 12 ya kwanza uwezo wa kuzuia ujauzito ni 95% ila ukinywa siku ya tatu baada ya masaa 48 ni 58% tu. Hivyo ni vizuri kuwahi..

Tahadhari
Hii sio njia ya uzazi wa mpango... ni vyema kutumia njia za uzazi wa mpango za kawaida kama mipira ili pia tujikinge na maradhi ya zinaa..

Pili hutakiwi kutumia njia hii zaidi ya mara moja kwa mwezi madhara yake unaharibu balance ya homoni na utableed sana na mzunguko wako utakuwa haueweki na pia unaweza pata machunusi usoni na ngozi kuwa na mafuta yaliyozidi.

Tatu ni gharama. Kwa dsm gharama yake inarange kuanzia 5000 mpaka 10000 hii ni kubwa sana ukizingatia bei ya kondomu au njia ya kudum ya uzazi wa mpango ambazo ni bure

"Be healthy and happy"

Nawapenda sana

Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swal lako kupitia whatsap no 076757271 jinalako litakua siri

kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo  https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU


@dr.ibu

Mdogo wangu alitoboa masikio na sindano masikio yametoka uvimbe je dawa yake ni nin?

 JIBU
 la sikio kwanza nakushauri asitibu kienyeji sana aende hospital Kutibu hapo inategemeana na ukubwa wa uvimbe... kama ni mdogo sana atapewa antibiotics na za maumivu tu atapona kama ni mkubwa atapasuliwa utakamuliwa atapewa dawa za maumivu na antibiotics

 Lakini tujifunze nini imetokea kwenye sikio lake.....kwenye ngozi kuna wadudu wengi sana ikiwemo bacteria.... bacteria maarufu zaidi anayeishi kwenye ngozi ni staphylococcus aureus anaishi bila kusababisha shida yoyote kama (normal flora)mpaka akiingia kwenye sehemu nyingine ya mwili ndio husababisha shida huyu ndio husababisha majipu na miwasho na vipele vingi kwenye ngozi... sasa mtu ukijitoboa ngozi au kwa hapo kutoga masikio bila kusafisha lile eneo kwa dawa au spirit unampa uwezo wa kuingia kwenye sehemu ya ndani anayoweza kuleta madhara...ndio maana kabla ya upasuaji huwa tunasafisha ngozi yote kwa iodine ili kuua kwanza hawa wadudu.... na tunaosha mikono kwa dawa maalumu pamoja na kuvaa gloves maalumu kuzuia wadudu hawa wasilete madhara lakini pia tunaongeza na antibiotics za kutumia ili hata kama wameingia wafe na ile dawa
MAADA 1.

MZUNGUKO WA KAWAIDA WA MWANAMKE.

Unapozungumzia afya ya binadamu wa kike huwezi kuacha kitu muhimu kuliko vyote ambacho ni mzunguko wake wa hedhi. Je ipi ni kawaida na ipi si kawaida na je ni vitu gani vinasababisha isiwe kawaida na magonjwa ambayo huambatana na mzunguko wa hedhi usio wa kawaida.    Kwa kawaida binadamu wa kike hupata hedhi ya kwanza akiwa na umri wa miaka 13-17 lakini chini ya miaka 12 na baada ya miaka 17 ndio tunamuweka kwenye group la aidha kawahi mno au kachelewa kupata hedhi. Baada ya hapo huanza kupata hedhi kila baada ya siku 21 mpaka 35 ( utafiti mpya unasema kawaida ni siku 22-38 bado ni kawaida) na kila kwenye mzunguko anapata hedhi kwa siku 3-7 ( utafiti mpya hadi siku 8 ni kawaida na chini ya siku 2 inakuwa sio kawaida). Hivyo basi hali yoyote ambayo itakuwa kinyume na hapo inaweza kuwa inaambatana na magonjwa. Mzunguko huu hudhibitiwa na homoni za kike ambazo hutolewa na kudhibitiwa na ovari na ubongo.   
Matatizo ya hedhi ambayo yapo sana mazingira yetu ni kama ifuatavyo:

1. Maumivu wakati wa hedhi(dymenorrhea)

Maumivu wakati wa hedhi huwata wadada na wamama wengi. Tafiti nyingi zimefanyika kuhusu tatizo hili na inaonekana inatokana na vitu vingi ila mojawapo ni kuvutana kwa kuta za mji wa uzazi (uterus) na dalili zake ni maumivu ya tumbo,  mgongo na kiuno. Utafiti uliofanywa dar es salaam ulionesha wanafunzi asilimia 76 wa sekondari wanatatizo hili. Lakini habari njema ni kuwa asilimia kubwa ya watu maumivu huwa yanapungua kadri umri unavoongezeka. Na mpaka anapozaa mtoto wa kwanza asilimia kubwa maumivu huwa yanapotea kabisa.  Dawa yake ni kutumia dawa za maumivu kuanzia panadol, diclofenac, ikizidi sana huwa inakuwa imetokana na hormone zinakuwa zimezalishwa kwa wingi mno kwahiyo unapewa dawa za kubalanzi homoni ambazo ni vidonge vya uzazi wa mpango kwa siku 28 baada ya hapo unakuwa poa.

2. Kupata damu nyingi.

Hapa ni either kupata damu zaidi ya siku 8 au damu inatoka nyingi sana kwa siku mpaka mtu anakosa nguvu, kupoteza fahamu, kuumwa sana na kichwa kusikia mapigo ya moyo yanaenda mbio, kupata taabu kupumua na kwenda kuongezewa damu wakati mwingine. Na mara nyingi damu hutoka mfumo wa mabonge mabonge(clots).  Damu ya hedhi kawaida ni isizidi mills 80 ( chupa ya soda ina 350 mls).
Mara nyingi watu hawa huweza kupata damu katikati ya mzunguko maana yake kabla siku za kupata hedhi yake anapata katikati na siku zake zikifila tena anapata kama kawaida. Hii husababishwa na magonjwa mengi ikiwemo
Polyp-kwenye mji wa uzazi kuna kuwa na uvimbe ambao sio kansa

Fibroid-huu pia ni uvimbe lakini utofauti na polyp  ni kuwa poly inakuwa kama vidole na pia vinavyochomoza kwenda katikati ya uterus.