Wednesday, 19 September 2018
SWALI:Nina shida naomba unisaidie..... Nilikua mjamzito early pregnancy ila jumatatu iliyopita nilifanya kaz ngumu ucku wake nkatokwa na dam nying sana nlienda hospital nkaambiwa mimba imetoka nlioshwa nkapewa dawa pamoja na sindano.... Dam ilikata kwa mda ila juz nliumwa sana na kutokwa na dam upya ila ikakata leo hali ileile imenirudia naomba nisaidie
JIBU: Pole sana mom/dada... damu haitakiwi kuendelea kutoka ukiwa umeshasafishwa... uwezekano ni vitu viwili ni aidha ilibakia hawakumaliza kitu ambacho uwezekano ni mdogo kama ikifanyika hospitali au kuna ugonjwa unaitwa GTD ( Gestational Trophobastic Disease) ambao unaendelea kuwa na dalili za ujauzito hata kama mimba imeshatoka. Na ukipima mkojo kipimo cha mimba kinakuwa positive. Kawaida mimba ikishatoka baada ya siku 14 kipimo cha ujauzito kile cha mkojo kinatakiwa kuwa negative lakini kwa hawa bado kinakuwa positive..
Chakufanya nakushauri nenda hospitali ya karibu kubwa ya wilaya, au mkoa au rufaa kaonane na daktari.. Utapigwa utrasound ambayo itaonesha vyote kama bado kuna mabaki ya mimba au huo ugonjwa wa GTD na pia utaangaliwa kama una upungufu wa damu na kama umepata maambukizi (infection) yoyote kwa kupima damu yako. Alafu baada ya siku 14 kuisha unaweza kupima kipimo cha ujauzito kama nilivoeleza pale juu. Pole sana mungu akusimamie upone. Alafu pia mimba ikitoka ni rahisi sana kupata mimba nyingine haraka sana kwa hiyo tunashauri watumie njia za uzazi wa mpango... na njia nzuri kwao ni loop ambayo unaweza kutoa na ukapata mimba muda wowote bila kusubiri kama sindano
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment