Wednesday, 19 September 2018

SWALI:Doctor samahani naomba kuuliza swali. ninapokuwa natoa haja kubwa mgongo/kinyama kinatoka,sipati mauivu yoyote ila lazima nikirudishe kwa kidole naomba kujua nini hiki na kama kina athari kiafya

JIBU
Ugonjwa wako unaitwa bawasiri
Bawasili au hemorrhoids kitaalamu

Ni ugonjwa ambao hutokana na kuvimba kwa mishipa ya damu ambayo ipo sehemu ya chini ya njia ya haja kubwa(mkundu)

 Mishipa hii huvimba taaratibu na damu yake huweza aidha kuganda( thrombosed) au kuathiriwa na wadudu ( infected) na hapo ndio huwa na maumivu lakini la sivyo huwa haiumi.

Bawasiri zimegawanyika makundi mawili zipo ambazo hukaa ndani kabisa (internal hemorrhoids) na nyingine huwa zinakuwa nje na kwa juu zinakuwa zimevikwa ngozi ya kawaida pale kwenye mlango wa kuingilia (external hemorrhoids )...

NINI HUSABABISHA.
sababu kubwa ya kupata bawasiri ni hali ya wima ya binadamu tuliyonayo ambayo inasababisha damu inayoenda eneo la chini ya mwili kama miguu kutokana kushindwa kupanda juu kirahisi hii ndio sababu wanyama kama mbuzi, mbwa ambao hawapo wima hawapati hemorrhoids, damu isipopanda haraka inasababisha mishipa ile kutanuka na kuvimba na ndio tunaita hemorrhoids.

2. Kupata choo kikavu/ kigumu sana kutokana na kutokunya maji ya kutosha na vyakula vyenye nyuzi kama mboga za majani na matunda. Hii husababisha kubanwa kwa mishipa ya damu na kuzuia damu kupanda juu kurudi kwenye moyo na hivyo huleta uvimbe...

3. Kuwa na pressure kubwa tumboni...

Hii huzuia pia damu kurudi juu kwenda kwenye moyo kirahisi..hii huwapata watu  wenye uvimbe tumboni, au wajawazito, wanaofanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito na hao wenye constipation( choo kigumu) pia wazee wenye tezi dume au kansa ya kibovu cha mkojo

Zipo sababu nyingi lakini hizo ndio ambazo ni muhimu sana kwenu.


Dalili zake .
1. Kuhisi kuna kitu kipo ndani ya sehemu ya haja kubwa ambacho hakitoki
 Hisia hii huwa inategemeana na ukubwa wa uvimbe.
2. Huweza kutoka damu wakati wa kutoa haja kubwa
3. Maumivu wakati wa kutoa haja kubwa.
4. Kuhisi kuna kitu kinatoka na kurudi wakati wa kutoa haja kubwa.
5.kuona kabisa uvimbe umetokezea kwenye njia ya haja kubwa.

NB:uvimbe unaweza ukawa mmoja au zaidi ya mmoja. Mara nyingi hukaa sehemu kama ni saa ni sehemu ya saa 4, 7 na 11.

GRADE ZAKE..
1. Kunakuwa na uvimbe mdogo kwa ndani
2.uvimbe unakuwa unaweza kutoka nje mtu akijikamua tumbo na kurudi wenyewe akiacha kujikamua
3.uvimbe unakuwa unatoka mtu akijikamua na unaweza kurudishwa kwa kitu choxhote kama kidole na ikawezekana kukaa ndani

Grade 4. Unakuwa umetoka nje na hauwezi hata kurudishika ndani

MATIBABU NA NJIA ZA KUJIKINGA
 Matibabu yanategemeana na grade ya bawasiri.

Grade 1. Kuna dawa ambayo huwa tunachoma ambayo inakausha kabisa
Grade 2. Kuna ruber band wanaifunga kwa sehemu inapoanzia uvimbe(shina lake) alafu uvimbe wote unakauka kwa sababu unakosa damu

Au kuna kifaa kinaitwa stapler kinatumika kukata bawasiri mojamoja.

Grade 4 tunafanya operation  na kuna aina nyingi za operation.

Namna ya kujikinga.

1.kunywa maji ya kutosha
2.kula vyakula vya nyuzi nyuzi
3. Acha kunyanyua vyuma fanya mazoezi ya kawaida
4.fanya mazoezi kupunguza mwili
5. Usikae sana chooni.. kupokea simu au kusoma gazeti au kuchati chooni

6.tibu haraka kama una choo kigumu

7. Acha kujikamua wakati wa kukojoa au kutoa haja kubwa.

8. Ukijisikia haja kubwa usiibane nenda.
By @dr.ibu

No comments: