MAJIMAJI NA HARUFU KWENYE UKE
Ute kwenye uke ni nini? — hili ni neno ambalo hutumika na wataalamu wa afya kuelezea maji maji yanayokuwa au kutoka katika sehemu za siri za mwanamke au uke"Vaginal discharge"
Maji maji haya ni muunganiko wa seli za mwili hasa za kuta za uke na shingo ya kizazi pamoja na bakteria ambao huishi kwenye uke.
Je hii hali inaweza kuwa ya kawaida? — Ndio kwa mwanamke ambaye hana tatizo lolote maana yake anapata hedhi ya kawaida huwa anakuwa na ute huu au majimaji haya lakini ni kiasi kidogo
Kwa kawaida ute au majimaji haya huwa ni meupe au clear kama maji au mazito mazito ila huwa hayatoi harufu yoyote.
Wanawake wanatofautiana
Katika kiasi cha majimaji ambayo huwa yanakuwa kwenye uke wengine huwa wanakuwa na kiasi kikubwa wengine kidogo sana.
Pia mwanamke mmoja anaweza akawa na kipindi kingine anakuwa na majimaji mengi na wakati mwingine kidogo.
Mf. Mwanamke anakuwa na maji mengi zaidi:
●akiwa mjamzito
●akitumia dawa za uzazi wa mpango
●wiki mbili kabla hajaanza period. Ni kipindi yai linatoka kwenye ovari
Pia wanawake ambao wamefika umri wa kutoona siku zao( menopause) huwa wanakuwa na ute kidogo au uke unakuwa mkavu kabisa.
Je majimaji kwenye Uke yanaweza kuwa ni ugonjwa?
NDIO... majimaji kwenye uke yanaweza kuwa ni ugonjwa endapo yataambatana na vitu vifuatavyo:
●muwasho sehemu za siri
●wekundu, maumivu au uvimbe sehemu za siri
●majimaji ambayo ni ya njano au kijani au yanachanganyikana na damu
●majimaji yakiwa yanatoa harufu kali
●kupata maumivu unapokojoa au unapojamiiana
●kupata maumivu chini ya kitovu
●joto kupanda au kuchemka mwili(homa)
NINI HUSABABISHA MAJIMAJI KUTOKA KWENYE UKE KAMA UGONJWA:
Visababishi ni vingi sana ila mara nyingi ni
●mambukizi kwenye uke
Kuacha vitu kwenye uke kama pad au condom
● kutumia sabuni au vitu kemikali nyingine kwenye uke
●homoni kutobalance
NoTE. Ukiona dalili kama hizi usikimbilie kununua dawa na kumeza kwa sababu vyanzo ni vingi nenda hospitali kamuone daktari wako mueleze.
Daktari atachukua majimaji haya atayapima na kugundua chanzo na utapata dawa kutokana na chanzo cha tatizo..usitumie mitishamba ya insta tatizo linaweza kuzidi kuwa kubwa. Hakuna upasuaji.
Kama majimaji haya yanatokana na maambukizi ya ugonjwa fulani nashauri usifanye mapenzi pia ni vizuri kquongea na mwenzi wako mtibiwe pamoja..
Acha kufanya mapenzi ukiwa unatoa majimaji ambayo sio ya kawaida au yanatoa harufu mpaka ujue kuwa hauna maambukizi ya ugonjwa .
NAMNA YA KUZUIA KUTOKA MAJIMAJI KWENYE UKE AMBAYO SIO YA KAWAIDA AU YENYE KUTOA HARUFU
●Tumia maji ya uvuguvugu
Na sabuni ambayo haitoi harufu yoyote kuosha sehemu zako za siri.sehemu ya juu ya uke
●kuoga maji ya uvuguvugu na usitumie sabuni ambazo zina harufu
.Usitumie spray au poda au perfume kwenye sehemu za siri
●usiingize kitu chochote iwe kidole au kusafisha ndani ya uke kwa njia yoyote ile wala usiingize maji kwenye uke
●baada ya kumaliza haja chooni usitumie karatasi toilet paper zenye harufu au manukato yoyote.
TIBA
Majimaji au harufu kwenye uke inatibiwa kutokana na kisababishi ambacho hupatikana baada ya kuchukua majimaji haya na kuyapeleka maabara kisha kujua chanzo hasa na mdudu hasa aliyesababisha ndipo utapewa dawa.
Itaendelea
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri
kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU
Be healthy and happy
No comments:
Post a Comment