Ili kujua kuwa ni kweli mtu kabakwa au hamna hasa kwa wanawake basi kuna vitu vingi.
1. Uwepo wa michubuko sehemu za siri nje au ndani ya uke.
Ikumbukwe kuwa mtu anayebakwa mara nyingi haandaliwi kihisia kwa hiyo ni rahisi kuchubuka na pia sehemu ya nje ya uke mf.mashavu na kinena huwa kinavimba kwa kuumizwa.
2.uwepo wa shahawa ndani ya uke.
Hii inaweza kutumika endapo kosa hili limetendeka ndani ya siku 3 za mwanzoni lakini ina mapungufu mengi mfano:
a) kuna watu wanamwaga majimaji ambayo hayana mbegu za kiume kwa hiyo hautakuta kitu au ni chache sana kwahiyo ndani ya masaa kadhaa hutakuta mbegu yoyote ilobakia.
b) kuna watu wamekata mirija inayoleta mbegu za kiume kwenye uume kama njia ya uzazi wa mpango ko wao hawatoi mbegu wanatoa majimaji tu.
c) kuna watu wengi hasa wazee ambao walishakuwa na kansa ya tezi dume wanafanyiwa upasuaji wa kutoa korodani zote mbili na hivyo hawawezi kutoa mbegu za kiume.
d)kuchelewa kufika kituo cha huduma ndani ya huo muda.
e) matumizi ya kinga kama kondomu na dawa za kuulia mbegu (spermicide)
MHUSIKA ATATHIBITISHWAJE
kwa kutumia DNA inayoweza kupatikana kwenye vyanzo mbalimbali kama nywele za sehemu za siri, shahawa,pamoja na mabaki yanayopatikana kwenye kucha za mwanamke katika harakati za kujinasua, mara nyingi wanawake hutumia kama silaha hata kama ni fupi lakini sampuli inayotakiwa ni kidogo sana kwahiyo usipuuze.
KAZI YA DAKTARI AU MHUDUMU WA AFYA
a)kumhudumia mgonjwa aliyepata na tukio hilo kwa usiri na kutotangaza
b) kukusanya na kutunza ushahidi wote kwa sababu hii ni kosa la kisheria
C) kutoa ushahidi wa kitaalamu mahakamani kwa maandishi
d) kushauri kuripoti katika vyombo vya dola kuhusiana na matukio ya aina hii.
HUDUMA ZA KIAFYA ZINAZOTOLEWA KWA MTU ALIYEBAKWA.
1. Kutibu majeraha kama michubuko na vidonda
2.kumsaidia kisaikolojia kumuondolea msongo wa mawazo na ikiwezekana kumpa dawa zitakazosaidia kuondoa woga na msongo wa mawazo na kumchunguza kama yupo katika hatari ya kujiua.
3.kuzuia mimba. Akipimwa akikutwa hana mimba ndio anapewa njia za kuzia mimba ila kama anayo anakuwa aliipata kabla ya kubakwa.Hapa inategemea kaja siku ngapi baada ya kubakwa. Akija ndani ya masaa 72 au siku tatu anapata P2 kuzuia mimba akija kuanzia siku 4 mpaka 10 anapewa loop (kitanzi). Akija baada ya hapo kwa nchi nyingine anapimwa akiwa mjamzito mimba inatolewa. Kwetu sheria ya kutoa mimba hairuhusu hiki kipengele bado.
4. Kuzuia magonjwa ya ngono
Atapewa antibiotics kuzuia magonjwa kama gonorrhea kaswende na klamidia.
5. Kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kwanza mtu huyo atapimwa kwanza akikutwa na maambukizi maana yake alishakuwa amepata kabla ya kubakwa kwa hiyo atapelekwa CTC kuanza matibabu kwa sababu kipimo hakiwezi kusoma maambukizi uliyoyapata kwa muda mfupi kiasi hicho. Kama hana maambukizi anapewa dawa ya kuzuia kuambukiwa kwa sababu hatujui aliyembaka alikuwa ameathirika au alikuwa mzima. Atatumia kwa siku 28 alafu atapimwa tena.
NAMNA GANI YA KUTUNZA USHAHIDI NA KUFANYA MTU AKIBAKWA.
1. Kuwahi mapema hospitali hii itasaidia kupata ushahidi wa kutosha, kuzuia mimba, magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI
2.usioge au kujisafisha kwa njia yoyote ile
3.usibadilishe nguo au ukibadilisha fika nazo ulizovaa hospitali zihifadhiwe
4.usinyoe
5. Sema na watu jieleze usiogope usije ukapata msongo wa mawazo ambao unaweza kupelekea kujiua.
Mwandishi Dr.ibu.
No comments:
Post a Comment