NINI CHA KUFANYA MIMBA IKITOKA AU BAADA YA KUTOA MIMBA..
Baada ya mimba kutoka au mimba ikitoka kutokana na sababu mbalimbali iwe umekunywa dawa bila kujua au kwa kujua zikasababisha mimba kutoka basi kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa kuzingatia...kwanza kama ndio umeona damu tu imetoka nenda hospitali mara moja kwa sababu damu ikitoka sana inasababisha upungufu wa damu na moyo huwa unaweza kufeli... pia unatakiwa kuhakikisha hakuna mabaki ya kiumbe au masalia ya damu yanayobaki kwenye mfuko wa uzazi na njia pekee ni kwenda hospitali kusafishwa kizazi.. lakini pia unatakiwa kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya bacteria.. hii ni kutokana na kwamba mlango wa shingo ya kizazi upo wazi baada ya mimba kutoka hivyo inakuwa kwenye hatari ya kupata infection....ko unapata antibiotics angalau siku 7 mpaka 10.... tatu ni kutafuta chanzo cha mimba kutoka kama mimba imetoka inaweza sababu iliyosababisha mimba moja kutoka ikasababisha mimba inayofuata pia ikatoka... hivyo ni vizuri kutafuta chanzo ili kutibiwa kabla ya kupata mimba nyingine..
Nne ni uzazi wa mpango..
Ni rahisi zaidi mtu kupata mimba baada ya mimba kutoka pindi tu atakapofanya mapenzi...
Hivyo sio lazima aanze kupata mzunguko wake ndio awe katika hatari ya kupata ujauzito. Hatari yake ni kuwa chanzo chake cha mimba kutoka kinaweza kusababisha mimba kutoka tena na pia via vyake vya uzazi vinakuwa havijatengamaa kupata nguvu ya kubeba mimba tena kitu ambacho ni hatari kwa mama na mtoto aliyepo tumboni... hivyo tunashauri mama asijihusishe na kufanya mapenzi baada ya mimba kutoka au kuzaa mpaka siku 42 zitimie wiki 6 au mwezi mmoja na wiki mbili... lakini tunashauri aipate mimba mpaka angalau miezi mitatu mpaka sita baada ya kupoteza mimba...
Nini madhara ya kufanya mapenzi mapema mara tu baada ya mimba kutoka au kuzaa.?
See me at www.ibumd.blogspot.com kwa muendelezo
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri
kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU
Be healthy and happy
No comments:
Post a Comment