Swali.Nina ujauzito wa mwez mmoj na nusu lakn tumb linauma afu nakosa hamu ya kula
JIBu: Leo naomba tuelewane ujauzito huleta upungufu kidogo wa kinga mwilini ili mtoto aweze kukaa tumboni kwa sababu la sivyo kinga ya mwili itaua mtoto... kwa sababu mtoto aliyepo tumboni huwa anakuwa kama kitu au kiumbe kigeni ambacho hakikutakiwa kuwepo.. hivyo kinga ya mwili inapopungua unakuwa katika hatari ya kupata magonjwa tofauti na mtu wa kawaida.. na ukipata ugonjwa utakuwa wa nguvu zaidi na dalili zake zinakuwa kali zaidi kuliko ambaye hana ujauzito... magonjwa ambayo yanawashambulia sana ni UTI na malaria.. ndio maana tunashauri utumie dawa za malaria Sp na ulale kwenye NET kila siku.. lakini kwako nadhani utakuwa na UTI ambayo dalili zake ni..
1. Kuumwa tumbo hasa chini ya kitovu
2.homa na mwili kuchoka
3.kichwa kuuma na wakati mwingine kukosa hamu ya kula
4.maumivu unapokojoa
5.kukojoa mara kwa mara
Kwa mjamzito inatia changamoto kwa sababu anakojoa mara kwa mara kawaida kwa sababu ni mjamzito lakini pia akikosa hamu ya kula,homa, na kichwa kuuma inaweza kuwa malaria na kwa sababu hajaanza dozi ya dawa za kuzuia malaria.
Kujua ni kutumia kipimo kupima malaria na UTI kujua nani anakusumbua japo kwa sababu tumbo linauma more likely utakuwa na UTI maabukizi kwenye njia ya mkojo.
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 0767357271 jina lako litakua siri
kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU
Be healthy and happy
No comments:
Post a Comment