Wiki ya kansa ya matiti duniani...
Kansa ya matiti ni kati ya kansa au saratani ambazo zipo juu katika kuathiri afya ya wanawake duniani..kwa Tanzania ni ya pili ikitanguliwa na kansa ya shingo ya kizazi.
Hii huanza kama uvimbe ambao huwa hauonekani bali mtu anaweza kuuhisi akiwa anaoga au kujigusa au wakati mwingine mtu mwingine anaweza kuuhisi akiwa anagusa titi lake..
Hukua haraka na huweza kusababisha titi kuvimba, kubadilika rangi, baadae ngozi yake kuwa kama ganda la chungwa..lakini pia huweza kutokea kidonda ambacho hakina maumivu au unaweza kushangaa titi halichezi linakuwa linashikana na kifua hata ukiinama halichezi... baadae mtu huweza kuwa na mitoki ikiwa kwapani ikivimba au kuwa na vidonda.. baadae kansa hii huweza kusambaa sehemu mbalimbali mwilini ikiwepo mifupa hasa ya mgongoni mtu anakuwa na maumivu ya mgongo na kiuno na wakati mwingine kuvunjika hata akidondoka kidogo tu.. kwenye ubongo ambapo mtu huwa anaweza kuwa kama na kifafa, kichwa kuuma sana hasa asubuhi na pengine kupoteza fahamu na kupoteza kumbukumbu...kwenye mapafu anakuwa anashindwa kupumua vizuri, kokohoa damu, na kifua kubana au kuuma... pia tumbo linaweza kujaa maji na kuvimba sana..
Saratani hii kama kansa nyingine chanzo hasa hakijulikani isipokuwa kuna vihatarishi ambavyo mtu akiwa navyo basi anaweza kuwa kwenye hatari ya kupata kansa ya matiti
1.sigara na pombe
2.uzito mkubwa
3.kama mtu kwenye familia aliwahi kuwa ugonjwa huu..wengine pia wanakuwa kwenye hatari... na kama alikuwa na kansa kwenye matiti yote mawili hatari inaongezeka pia kama aliipata akiwa na umri wa chini ya miaka 50 hatari inakuwa kubwa zaidi
4.utoaji wa mimba.. pia mimba inavozidi kuwa na miezi mingi ikitolewa au ikitoka hatari inazidi kuongezeka
5.kama ulishawahi kupata kansa hii unakuwa katika hatari ya kupata tena mara ya pili hata ukipona.
6.kuwa na uvimbe wowote kwenye ziwa kunakuweka katika hatari ya kupata kansa ya ziwa
7.kutokuwa na mtoto mpaka miaka 35 ndio maana zamani ulikuwa unajulikana kama ugonjwa wa masister
8.kuvunja ungo mapema kabla ya miaka 12
9.kuwa na watoto wachache kama mmoja pia ni hatari
10.kutumia dawa za homoni kwa wazee
NINI CHA KUFANYA
1.kagua matiti yako mara kwa mara unapooga
2.acha uvutaji wa sigara pia usikae na wavuta sigara,punguza uzito kwa kufanya mazoezi na punguza unywaji wa pombe
3.kama una ndugu alishawahi kuwa na ugonjwa huu fanya kipimo mamogram mara kwa mara angalau mara moja kwa miezi sita mpaka mwaka mmoja
4.ukihisi uvimbe ambao sio wa kawaida uwahi hospital haraka ukachunguzwe zaidi kumbuka inatibika ukiwahi.
Itaendelea
@dr.ibu
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri
kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU
Be healthy and happy
No comments:
Post a Comment