Tuesday, 18 September 2018

SWALI: Doctor samahani naomba kuuliza swali, nina mtoto binti wa shule nimemkuta na miso chumbani kwake je dawa hiyo ina kazi gani?

Miso kama jina maarufu ndugu alivouliza hiko ni kifupi tu ila inaitwa misoprostol...ni dawa inayotumika zaidi kuongeza contraction ( kujikunja kwa kuta za  mji wa uzazi) na ndio maana wengine wanazitumia katika kutoa mimba... pia hospital tunatumia kusafishia kizazi au kutoa mimba ambayo imefia tumboni... pia tunaitumia kuzuia damu kutoka kama mama katoa damu nyingi sana baada ya kujifungua na hayo yote yana dose tofauti... kuna namna tofauti na maarufu ni ile ya kuweka kwenye kuta za uke lakini ipo ya kumeza pia.

Ushauri ni kwamba ni kwamba kapime kama wanao ni mjamzito basi anawweza akawa alikuwa anataka kuitoa mimba. Pia ongea nae taratibu madhara  ya kutoa mimba na  kutumia dawa bila kuandikiwa na daktari


Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri

kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo  https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU


Be healthy and happy

Dr.ibu

No comments: