JIBU
kwanza kabisa pole kwa msongo mawazo ambao upo nao kwa sasa.
Ukitaka kujua baba a mtoto unataakiwa kujua siku zako za hatari za kutungishwa mimba katika mzunguko wako. Katika mzunguko wa kila mwanamke kuna sehemu mbili(2 phases).
Sehemu ya folicular ambayo ni sehemu ambapo yai linapitia mabadiliko mbalimbali ili liweze kurutubishwa. Katika hatua hii pia kunakuwa na maandalizi ya kuta za mji a uzazi (uterus) ka ajili ya mimba kutunga na kutunzwa kwa miezi tisa (wiki 36 hadi 40). Phase a folicular haina idadi kamili ya siku ila huanza siku ya kwanza mwanamke anapoanza mzunguko wake (siku ya kwanza ya hedhi) hadi siku yai linapotoka kwenye ovari (ovulation day). siku hii hutofautiana kutokana na urefu wa mzunguko wa mwanamke husika.
sehemu ya luteal
Au kitaalamu luteal phase hii huwa ni sawa kwa kila mwanamke. ni idadi a siku ambazo yai linaweza kuishi, hii huchukua siku 14 tu.
Kitu kingine cha msingi kujua ni kwamba mbegu ya kiume huweza kuishi kwa siku 2-3 (masaa 48-72) hivyo ukijamiiana siku tatu kabla ya yai kutoka litaikuta mbegu ya kiume na kuna uwezekano wa kurutubishwa na ukapata mimba.
Pia yai likishatoka kwenye ovari hukaa siku mbili mpaka tatu ndio hapo ukuta wake hua mgumu na mbegu haiwezi kutoboa ili kurutubisha. kwahiyo mtu akifanya mapenzi ndani ya muda huo ndio urutubishwaji hutokea
Mzunguko wa mwanamke unatofautiana ila wa kawaida ni kuanzia siku 21 hadi 35 hivyo basi hata siku zao za yai kutoka zinatofautiana isipokuwa tu luteal phase ambayo ni siku 14 hazibadiliki
ukitaka kujua siku ya yai kutoka unachukua idadi ya siku katika mzunguko unatoa 14 abazzo ni siku ambazo yai linaweza kuishi.
kwa swali la dada itakua 32-14 itakuwa 18. Kwahiyo siku yake ya yai kutoka inakuwa siku ya 18, ukiangalia tarehe tokea tarehe 6 siku 18 ni tarehe 23. kumbuka yai linakaa siku tatu na shahawa zinakaa siku 3 kwa hiyo kila aliyefanya naye mapenzi siku tatu nyuma au mbele ya tarehe 23 ni muhusika.Kwahiyo kuanzia wa tarehe 20 hadi 26 wote wamo katika siku hatari.
Boyfriend alikuwa naye tarehe 20 na tarehe 21 ni siku hatari na akachepuka tarehe 22 ambayo ni siku hatari zaidi.
Lakini ukitumia sayansi kwamba jinsi siku zinavozidi kwenda mbegu ya kiume hua inazidi kupoteza nguvu wa tarehe 22 anakuwa na uwezekano mkubwa zaidi kwa sababu mbegu zake zilikaa siku moja tu ndio yai likafika.
Hata ukiongeza na kwamba alikua anamwaga nje bado yeye ndio kuna uwezekano kubwa zaidi kwa sababu njia hii huwa sio effective sana. uwezekano wake wa kuzuia ujauzito ni chini ya 30%
Jibu kamili ni DNA.
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri
kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU
Be healthy and happy
Dr.ibu
No comments:
Post a Comment