Tuesday, 18 September 2018

SWALI:Doctor samahan mama angu anatatizo limesumbua kwa mrefu , anadai kila akila chakula na akinywa maji, maji hayo yanaenda kubana sehemu ya juu upande wa kushoto na wa tumbo mauvivu makali sana anayapata. tatizo lake ni nini?


 Ila nadhani anacho maanisha ni kwamba akila chakula anapata maumivu yanayokuwa makali yanakuwa kama yanaunguza na yanazunguka mgongoni pande zote .

Hii ni aina ya maumivu yanayotokana na vidonda vya tumbo...

Watu kama hawa huwa inafika kipindi hawagusi chakula kabisa kwa sababu ya maumivu...aina hii ya vidonda vinakuwa kwenye mfuko wa tumbo kabisa ( stomach ulcer). Hawa huwa wanakonda sana kutokana na kuacha kula sababu ya maumivu


Aina nyingine ya vidonda vya tumbo( PUD) hizi hukaa kwenye utumbo mdogo (duodenal ulcer) hizi huuma wakati wa njaa hivyo watu kama hawa huwa hawavumilii njaa. Wakati mwingine wanaamka kabisa usiku kutafuta chakula au kupika hata saa nane usiku wanakula sana na wananenepa kupindukia.

Dawa zao ni zilezile dawa tatu  antibiotic mbili na moja kwa ajili ya kuzuia asidi amoxicillin pantoprazole na metronidazole anakunywa kwa siku 14 au ananunua kuna package  ipo na zote inaitwa heligokit.



Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri

kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo  https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU


Be healthy and happy

Dr.ibu





No comments: