Monday, 17 September 2018

MAADA 1.

MZUNGUKO WA KAWAIDA WA MWANAMKE.

Unapozungumzia afya ya binadamu wa kike huwezi kuacha kitu muhimu kuliko vyote ambacho ni mzunguko wake wa hedhi. Je ipi ni kawaida na ipi si kawaida na je ni vitu gani vinasababisha isiwe kawaida na magonjwa ambayo huambatana na mzunguko wa hedhi usio wa kawaida.    Kwa kawaida binadamu wa kike hupata hedhi ya kwanza akiwa na umri wa miaka 13-17 lakini chini ya miaka 12 na baada ya miaka 17 ndio tunamuweka kwenye group la aidha kawahi mno au kachelewa kupata hedhi. Baada ya hapo huanza kupata hedhi kila baada ya siku 21 mpaka 35 ( utafiti mpya unasema kawaida ni siku 22-38 bado ni kawaida) na kila kwenye mzunguko anapata hedhi kwa siku 3-7 ( utafiti mpya hadi siku 8 ni kawaida na chini ya siku 2 inakuwa sio kawaida). Hivyo basi hali yoyote ambayo itakuwa kinyume na hapo inaweza kuwa inaambatana na magonjwa. Mzunguko huu hudhibitiwa na homoni za kike ambazo hutolewa na kudhibitiwa na ovari na ubongo.   
Matatizo ya hedhi ambayo yapo sana mazingira yetu ni kama ifuatavyo:

1. Maumivu wakati wa hedhi(dymenorrhea)

Maumivu wakati wa hedhi huwata wadada na wamama wengi. Tafiti nyingi zimefanyika kuhusu tatizo hili na inaonekana inatokana na vitu vingi ila mojawapo ni kuvutana kwa kuta za mji wa uzazi (uterus) na dalili zake ni maumivu ya tumbo,  mgongo na kiuno. Utafiti uliofanywa dar es salaam ulionesha wanafunzi asilimia 76 wa sekondari wanatatizo hili. Lakini habari njema ni kuwa asilimia kubwa ya watu maumivu huwa yanapungua kadri umri unavoongezeka. Na mpaka anapozaa mtoto wa kwanza asilimia kubwa maumivu huwa yanapotea kabisa.  Dawa yake ni kutumia dawa za maumivu kuanzia panadol, diclofenac, ikizidi sana huwa inakuwa imetokana na hormone zinakuwa zimezalishwa kwa wingi mno kwahiyo unapewa dawa za kubalanzi homoni ambazo ni vidonge vya uzazi wa mpango kwa siku 28 baada ya hapo unakuwa poa.

2. Kupata damu nyingi.

Hapa ni either kupata damu zaidi ya siku 8 au damu inatoka nyingi sana kwa siku mpaka mtu anakosa nguvu, kupoteza fahamu, kuumwa sana na kichwa kusikia mapigo ya moyo yanaenda mbio, kupata taabu kupumua na kwenda kuongezewa damu wakati mwingine. Na mara nyingi damu hutoka mfumo wa mabonge mabonge(clots).  Damu ya hedhi kawaida ni isizidi mills 80 ( chupa ya soda ina 350 mls).
Mara nyingi watu hawa huweza kupata damu katikati ya mzunguko maana yake kabla siku za kupata hedhi yake anapata katikati na siku zake zikifila tena anapata kama kawaida. Hii husababishwa na magonjwa mengi ikiwemo
Polyp-kwenye mji wa uzazi kuna kuwa na uvimbe ambao sio kansa

Fibroid-huu pia ni uvimbe lakini utofauti na polyp  ni kuwa poly inakuwa kama vidole na pia vinavyochomoza kwenda katikati ya uterus.

No comments: