Mazoea ni kwamba mtu akisema kizazi anamaanisha uterus..
Hii ndio mara kwa mara mnasikia mkipigwa utrasound huko wanakuambia una uvimbe kwenye kizazi. Watu wengi wakasema nizungumzie.
Sasa huu ni moja ya aina ya uvimbe ambao unakuwa kwenye kuta za kizazi/Uterus. Ni uvimbe ambao ndio unaongoza kati ya aina zote za uvimbe kwenye kuta za kizazi. Mungu mkubwa uvimbe huu sio kansa na uwezekano wa kuwa kansa ni mdogo sana ni chini ya 0.1% maana yake ni mtu mmoja kati ya watu wenye uvimbe 1000.
Inakadiriwa kwamba 20% ya wanawake wakifika umri wa miaka 30 basi wanakuwa wameshapata fibroid. Uzuri ni kuwa asilimia kubwa 50% huwa hawana dalili yoyote wako freshi tu na hauwasumbui hata kidogo.
Na uvimbe huu huwapata zaidi watu :
1.weusi kuliko wenzetu wa rangi nyeupe.
2.watu ambao hawana watoto au wenye ugumba wa mtoto mmoja. Maana yake ana mtoto mmoja lakini anajaribu kupata ujauzito tena hawapati.
3.umri ambao wanakuwa wengi wanapata ugonjwa huu ni miaka kati yaa 35 na 45.
4.urithi kifamilia kama kuna mtu ana uvimbe na wanawake wengine kwenye familia kuna uwezekano wa kuwa na uvimbe japo sio lazima.
Ukuaji wa uvimbe huu hutegemea homoni ya estrogeni.. ndio maana
1.Huwa unaongezeka kwa watu ambao bado wanaona siku zao wakishaacha kwenye miaka ya 50 unapungua na baadae unaweza kupotea kwa sababu estrogen inakuwa imepungua sana mwilini
2.unaongezeka zaidi kipindi cha ujauzito kwa sababu homoni inakuwa nyingi kwenye mwili.
3.Haiwezi kutokea kabla ya kubalehe/ Kuvunja ungo kwa sababu homoni pia zinakuwa kidogo.
4. Baada ya kuacha siku zake mwanamke hawezi kuota fibroid mpya na zilizokuwepo zinapungua au kupotea kabisa kwa kunyauka.
5.inawapata watu wanene zaidi kwa sababu mafuta huwa yanaweza kutengeneza hizo homoni kwenye mwili.
6. Watu wanaotumia dawa za uzazi wa mpango zenye homoni moja.Ila hizo ambazo mnatumia sana siku hizi hazina uhusiano na fibroid.
Fibroid inaweza ikawa moja au zaidi ya moja na ukuaji wake huwa hauwi sawa nyingine inaweza kukua haraka kuliko nyingine.
Uvimbe huu chanzo chake kamili hakijulikani kisayansi. Lakini kuna mawazo ya wanasayansi wengi wakisema unatokana na misuli ya kuta za uzazi kubadilika na kukua haraka zaidi ya kawaida na mwili kushindwa kuukontrol..
Kwa hiyo mgonjwa anakuja hospital anaweza kuwa na mtoto mmoja mkubwa kuanzia miaka 10 nakuendela au hana mtoto kabisa...
Japo wakati mwingine wengine wanaweza wakawa na watoto wengi lakink kama amezaa akiwa na umri mdogo na akazaa mara kwa mara anaweza akawa kwenye kundi hili hatarishi kupata fibroid...umri wa kati ya miaka 35 hadi 45.
Dalili za fibroid
Kama nilivosema zaidi ya 75% hazina dalili basi hugundulika kwa bahati tu kama hivo ukipiga utrasound au dr akiwa anagusa tumbo akaona kuna uvimbe.
Lakini kama dalili mara nyingi hutegemeana na ukubwa na sehemu ilipo.
1.kutoka damu nyingi ya hedhina inayoendelea kuzidi kila mzunguko. Hii ni kwa sababu inazuia kujiminya kwa mishipa ya damu ya kwenye kuta za kizazi ili damu isitoke.
2.mzunguko kuwa hautabiliki...kwenda hedhi mara nyingi zaidi ya kawaida.
3.maumivu wakati wa hedhi
4.maumivu wakati wa tendo
5.kushindwa kupata mimba
6.kupoteza mimba mara kwa mara kwasababu nafasi imejaa uvimbe kwahiyo mimba zinatoka
7.tumbo kuuma chini ya kitovu
8.kuvimba chini ya kitovu
![]() |
Mchoro kuonesha aina mbalimbali za fiboid kutokana na eneo zilipo |
No comments:
Post a Comment