Wednesday, 17 October 2018

"UKIBAKWA USIOGE, KUNYOA NYWELE WALA KUKATA KUCHA" DR.IBU

USHAHIDI WA KITAALAMU KWA ALIYEBAKWA.

ushahidi wa kitaalamu kwa aliyebakwa kuhusiana na mtuhumiwa aliyembaka unakusanywa na daktari kujua endapo  ni kweli mtu huyu kabakwa au sio kweli.
Ili kujua kuwa ni kweli mtu kabakwa au hamna hasa kwa wanawake basi kuna vitu vingi.
1. Uwepo wa michubuko sehemu za siri nje au ndani ya uke.
Ikumbukwe kuwa mtu anayebakwa mara nyingi haandaliwi kihisia kwa hiyo ni rahisi kuchubuka na pia sehemu ya nje ya uke mf.mashavu na kinena huwa kinavimba kwa kuumizwa.

2.uwepo wa shahawa ndani ya uke.
Hii inaweza kutumika endapo kosa hili limetendeka ndani ya siku 3 za mwanzoni lakini ina mapungufu mengi mfano:

 a) kuna watu wanamwaga majimaji ambayo hayana mbegu za kiume kwa hiyo hautakuta kitu au ni chache sana kwahiyo ndani ya masaa kadhaa hutakuta mbegu yoyote ilobakia.

b) kuna watu wamekata mirija inayoleta mbegu za kiume kwenye uume kama njia ya uzazi wa mpango ko wao hawatoi mbegu wanatoa majimaji tu.

c) kuna watu wengi hasa wazee ambao walishakuwa na kansa ya tezi dume wanafanyiwa upasuaji wa kutoa korodani zote mbili na hivyo hawawezi kutoa mbegu za kiume.

d)kuchelewa kufika kituo cha huduma ndani ya huo muda.

e) matumizi ya kinga kama kondomu na dawa za kuulia mbegu (spermicide)

MHUSIKA ATATHIBITISHWAJE

kwa kutumia DNA inayoweza kupatikana kwenye vyanzo mbalimbali kama nywele za sehemu za siri, shahawa,pamoja na mabaki yanayopatikana kwenye kucha za mwanamke katika harakati za kujinasua, mara nyingi wanawake hutumia kama silaha hata kama ni fupi lakini sampuli inayotakiwa ni kidogo sana kwahiyo usipuuze.

KAZI YA DAKTARI AU MHUDUMU WA AFYA

a)kumhudumia mgonjwa aliyepata na tukio hilo kwa usiri na kutotangaza

b) kukusanya na kutunza ushahidi wote kwa sababu hii ni kosa la kisheria

C) kutoa ushahidi wa kitaalamu mahakamani kwa maandishi

d) kushauri kuripoti katika vyombo vya dola kuhusiana na matukio ya aina hii.

HUDUMA ZA KIAFYA ZINAZOTOLEWA KWA MTU ALIYEBAKWA.
1. Kutibu majeraha kama michubuko na vidonda
2.kumsaidia kisaikolojia kumuondolea msongo wa mawazo na ikiwezekana kumpa dawa zitakazosaidia kuondoa woga na msongo wa mawazo na kumchunguza kama yupo katika hatari ya kujiua.

3.kuzuia mimba. Akipimwa akikutwa hana mimba ndio anapewa njia za kuzia mimba ila kama anayo anakuwa aliipata kabla ya kubakwa.Hapa inategemea kaja siku ngapi baada ya kubakwa. Akija ndani ya masaa 72 au siku tatu anapata P2 kuzuia mimba akija kuanzia siku 4 mpaka 10 anapewa loop (kitanzi). Akija baada ya hapo kwa nchi nyingine anapimwa akiwa mjamzito mimba inatolewa. Kwetu sheria ya kutoa mimba hairuhusu hiki kipengele bado.

4. Kuzuia magonjwa ya ngono
Atapewa antibiotics kuzuia magonjwa kama gonorrhea kaswende na klamidia.

5. Kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kwanza mtu huyo atapimwa kwanza akikutwa na maambukizi maana yake alishakuwa amepata kabla ya kubakwa kwa hiyo atapelekwa CTC kuanza matibabu kwa sababu kipimo hakiwezi kusoma maambukizi uliyoyapata kwa muda mfupi kiasi hicho. Kama hana maambukizi anapewa dawa ya kuzuia kuambukiwa kwa sababu hatujui aliyembaka alikuwa ameathirika au alikuwa mzima. Atatumia kwa siku 28 alafu atapimwa tena.
NAMNA GANI YA KUTUNZA USHAHIDI NA KUFANYA MTU AKIBAKWA.
1. Kuwahi mapema hospitali hii itasaidia kupata ushahidi wa kutosha, kuzuia mimba, magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI
2.usioge au kujisafisha kwa njia yoyote ile
3.usibadilishe nguo au ukibadilisha fika nazo ulizovaa hospitali zihifadhiwe
4.usinyoe
5. Sema na watu jieleze usiogope usije ukapata msongo wa mawazo ambao unaweza kupelekea kujiua.

Mwandishi Dr.ibu.

Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

KIPIMO CHA KAMERA KUANGALIA NJIA KUBWA KINAFANYIKAJE?

SWALI; Daktari samahani nataka kujua, mdogo wangu anaumwa yupo hospitali, ugonjwa wake ni anapungukiwa damu mara kwa mara na hata akiongezewa inakaa kidogo anaongezwa tena. damu yake ni kundi O negative kwa hiyo ni taabu kupatikana. madaktari wamesema kesho anafanyiwa kipimo cha kuingiza kamera kwenye njia ya haja kubwa nina hofu sijui kinafanyikaje na madhara yake ni yapi?



JIBU: pole sana kwa familia na mgonjwa na pili nashukuru kwa kuleta swali lako ili pia wengine wajifunze...ni kweli damu group O negative ni ya watu wachache zaidina mbaya zaidi ni kwamba ni lazima ampate mwenye group O negative mwenzake ndipo anaweza kuongezewa damu. kuna vyama kabisa vya watu wenye damu group hilo sehemu nyingi dniani ili kusaidiana endapo mmoja akiwa anhitaji msaada wa damu. bahati mbaya hapa kwetu utaratibu huu haupo. Pia uhitaji wa damu ya kundi hili ni mkubwa kwa sababu hutumika zaidi mazingira ya wagonjwa wa dharura EMERGENCY DEPARTMENTS duniani kote kwa sababu unawza kumuongezea mtu yeyote hata kama hujui kundi lake a damu au huna mashine au muda wa kupima kundi lake la damu.

Tukirudi kwenye hiyo kipimo anachofanyiwa ndugu huyu kinaitwa colonoscopy. Hiki ni kifaa cha kisasa kabisa kinachotumika kuangalia utumbo mkubwa kama kuna vidonda au uvimbe au michubuko na kansa ya utumbo mkubwa. Kinatokana  na neno colon likimaanisha utumbo mkuwa na scopy nikuangalia. Hospitali kubwa hizi kama BUGANDO na MUHIMBILI na nyinginezo zinacho hichi kipimo.
Image
Mara nyingi watu wanafanyiwa colonoscopy wazee ili kuangalia kansa ya utumbo kuanzia miaka a 50 na kuendelea, inaweza kutumika kama njia ya uchunguzi tu mtu akiwa hana dalili kitaalamu tunaita screening ili kuiwahi kansa kabla haijasambaa, pia inatumika kuangalia ugonjwa unaitwa polyp ambazo ni uvimbe ambao unakuwa mithili ya vidole unakuwa kwenye utumbo na ni ugonjwa wa kurithi na ina nyingine za polyp hizi huwa zinakuja kubadilika na kuleta kansa au saratani. Kama mgonjwa akiwa na polyp kwa kutumia hiki kifaa daktari anaweza akazitoa wakati wa kufanya kipimo kitu ambacho kitapunguza uwezekano wa kupata kansa..
kuna njia nyingi za kugundua kama kuna kansa lakini waliowengi tunaona njia hii inakuwa rahisi zaidi kwa sababu inatoa uhuru wa kuona na kufanya matibabu kama kuchukua sampuli biopsy na kutibu kama kutoa polyp
Je kila mtu aende akafanyiwe colonoscopy? 
Tunashauri watu wafanye kama njia ya kuangalia kama wana magonjwa kama kansa ya utumbo mkubwa colonic cancer wakiwa na umri wa miaka 50 na kuendelea. Pia baadhi ya watu ambao wapo katika hatari ya kupata kansa ya utumbo mkubwa kama ambao katika familia kunamtu alishawahi pata huu ugonjwa kwa sababu huwa unarithishwa ko hawa wanaweza wakaanza wakiwa na umri mdogo hata 20.
sababu gani daktari ataamua kukufania colonoscopy?
kukiwa na damu kwenye kinyesi au kutoa tu dmu kwenye njia ya haja kubwa
kama utoaji choo wako unabadilika mara unaharisha unapata choo kigumu...yaani inabadilika kutoka ile kawaida yako
kupungukiwa damu mara kwa mara bila sababu inayojulikana mf. hujapata ajali 
Tumbo kuvimba au kuuma mud mrefu bila sababu ya msingi
kuhisi kama unajisikia haja imekubana na ukienda chooni unahisi kinyesi kimebakia ndani hakijaisha 
kama ulishawahi kuwa na kansa kabla au polyp kabla

Nini cha kufanya kabla ya colonoscopy? 
     Utaambiwa vyakula ambavyo unatakiwa kula na ambavyo hutakiwi kula. Mara nyingi nawaambia wagonjwa wale vyakula ambavyo hakiai sana tumboni wasile vyakula vyenye mafuta sana na mara nyingi wanywe maji ya kutosha na vyakula vyenye nyuzi nyuzi kama mboga majani na matunda siku moja kabla. Kuna dawa kama ulikuwa unazitumia unaweza kuzuliwa kutumia kwa sababu zitakuwa na muingiliano na kipimo. na utapewa karatasi yenye maelezo.Utumbo wote huwa unasafishwa kabla ya kufanya kipimo hiki ili kamera iweze kupita na daktari aweze kuona. hivyo utapea dawa ambayo itasafishautumbo na utaharisha kila kitu kitoke na inatakiwa unywe dawa yote utakayopewa na ni vizuri kumwambia daktari kama una hofu au shida yoyote katka maandalizi haya ili usiende kinyume.Kinavyofanyika kipimo hiki unapewa dawa ya usingizi ili uwe na amani na urelax na usiwe na maumivu, kisha inaingizwa kama kityubu ambacho kinakuwa na kamera kwa mbele na kisha unawashwa mwanga ndio daktari anakuwa anaona kwenye screen 
baada ya kipimo hiki unaweza kuendelea kula kama kawaida siku hiyo hiyo ila tunashauri usifanye kazi au kukaa sana unatakiwa kupumzika na utaanza kutumia dawa zako ambazo labda uliziacha ili kupisha kipimo.
ukiona yafuatayo unaweza kwenda hospitali baada ya colonoscopy.
kutapika
tumbo kuwa na maumivu makali
tumbo kuvimba na kuwa gumu au kujaa 
kutoka damu nyingi sehemu ya haja kubwa
kupata homa kali au kucemka mwili

Be healthy and happy


Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU

Nini husababisha majimaji na harufu kwenye uke?

MAJIMAJI NA HARUFU KWENYE UKE

Ute kwenye uke ni nini? — hili ni neno ambalo hutumika na wataalamu wa afya kuelezea maji maji yanayokuwa au kutoka katika sehemu za siri za mwanamke au uke"Vaginal discharge"
 Maji maji haya ni muunganiko wa seli za mwili hasa za kuta za uke na shingo ya kizazi pamoja na bakteria ambao huishi kwenye uke.

Je hii hali inaweza kuwa ya kawaida? — Ndio kwa mwanamke ambaye hana tatizo lolote maana yake anapata hedhi ya kawaida  huwa anakuwa na ute huu au majimaji haya lakini ni kiasi kidogo
Kwa kawaida ute au majimaji haya huwa ni meupe au clear kama maji au mazito mazito ila huwa hayatoi harufu yoyote.
Wanawake wanatofautiana
Katika kiasi cha majimaji ambayo huwa yanakuwa kwenye uke wengine huwa wanakuwa na kiasi kikubwa wengine kidogo sana.
Pia mwanamke mmoja anaweza akawa na kipindi kingine anakuwa na majimaji mengi na wakati mwingine kidogo.
Mf. Mwanamke anakuwa na maji mengi zaidi:

●akiwa mjamzito

●akitumia dawa za uzazi wa mpango

●wiki mbili kabla hajaanza period. Ni kipindi yai linatoka kwenye ovari

Pia wanawake ambao wamefika umri wa kutoona siku zao( menopause) huwa wanakuwa na ute kidogo au uke unakuwa mkavu kabisa.

Je majimaji kwenye Uke yanaweza kuwa ni ugonjwa?

NDIO... majimaji kwenye uke yanaweza kuwa ni ugonjwa endapo yataambatana na vitu vifuatavyo:

●muwasho sehemu za siri

●wekundu, maumivu au uvimbe sehemu za siri

●majimaji ambayo ni ya njano au kijani au yanachanganyikana na damu

●majimaji yakiwa yanatoa harufu kali

●kupata maumivu unapokojoa au unapojamiiana

●kupata maumivu chini ya kitovu

●joto kupanda au kuchemka mwili(homa)

NINI HUSABABISHA MAJIMAJI KUTOKA KWENYE UKE KAMA UGONJWA:
Visababishi ni vingi sana ila mara nyingi ni




●mambukizi kwenye uke

Kuacha vitu kwenye uke kama pad au condom

● kutumia sabuni au vitu kemikali nyingine kwenye uke


●homoni kutobalance


NoTE. Ukiona dalili kama hizi usikimbilie kununua dawa na kumeza kwa sababu vyanzo ni vingi nenda hospitali kamuone daktari wako mueleze.
 Daktari atachukua majimaji haya atayapima na kugundua chanzo na utapata dawa kutokana na chanzo cha tatizo..usitumie mitishamba ya insta tatizo linaweza kuzidi kuwa kubwa. Hakuna upasuaji.

Kama majimaji haya yanatokana na maambukizi ya ugonjwa fulani nashauri usifanye mapenzi pia ni vizuri kquongea na mwenzi wako mtibiwe pamoja..

Acha kufanya mapenzi ukiwa unatoa majimaji ambayo sio ya kawaida au yanatoa harufu mpaka ujue kuwa hauna maambukizi ya ugonjwa .

NAMNA YA KUZUIA KUTOKA MAJIMAJI KWENYE UKE AMBAYO SIO YA KAWAIDA AU YENYE KUTOA HARUFU

●Tumia maji ya uvuguvugu
Na sabuni ambayo haitoi harufu yoyote kuosha sehemu zako za siri.sehemu ya juu ya uke

●kuoga maji ya uvuguvugu na usitumie sabuni ambazo zina harufu

.Usitumie spray au poda au perfume kwenye sehemu za siri


●usiingize kitu chochote iwe kidole au kusafisha ndani ya uke kwa njia yoyote ile wala usiingize maji kwenye uke

●baada ya kumaliza haja chooni usitumie karatasi toilet paper zenye harufu au manukato yoyote.

TIBA
Majimaji au harufu kwenye uke inatibiwa kutokana na kisababishi  ambacho hupatikana baada ya kuchukua majimaji haya na kuyapeleka maabara kisha kujua chanzo hasa na mdudu hasa aliyesababisha ndipo utapewa dawa.

Itaendelea
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

Monday, 15 October 2018

Lini naruhusiwa kufanya mapenzi baada ya mimba kuharibika au baada ya kujifungua

Muendelezo:
UZAZI WA MPANGO KWA MTU ALIYETOKA KUTOA MIMBA AU MIMBA KUTOKA AU KUHARIBIKA..
kwanza unatakiwa kujua kuwa ni miiko ya kimaadili kwa daktari kujudge kuwa huyu mtu katoa mimba, kama kakosea au hamna sio kazi yake na wala hawezi kukuuliza wewe ukifika mwambie umetoa mimba unataka huduma atakuhudumia kama mtu au mgonjwa mwingine yeyote... pia ni kosa kisheria na kimaadili kushare taarifa za mgonjwa na hivyo ni sahihi nikisema kama ukiwa na miaka 16 na kuendelea siri zako hata mzazi wako hatajua ili mradi hutaki ajue.. hatutakiwi kureport kwenye vyombo vya dola ikiwa mtu kaja hospitali na katoa mimba kuomba msaada atajuana na mungu wake isipokuwa kama kuna kiasi kikubwa cha utoaji wa mimba katika jamii fulani daktari anawajibika kutoa taarifa ili elimu itolewe na pia hatatoa majina ya waliotoa mimba.. pia kuna sheria inayomzuia dr. Kutoa mimba ambayo haihatarishi uhai wa mama mjamzito japo kwa nchi nyingine kama ethiopia zambia south africa na nchi nyingi za magharibi wanasheria inayoruhusu kutoa mimba kama mtu kabakwa au anajua hawezi kutake care of the family. Najadili hili kwa sababu nimekutana na mabinti au wadada wengi wametoa mimba lakini wanaogopa kwenda hospitali mpaka wakati mwingine wanaogopa hata wanaombwa rushwa pengine au wanatumia gharama kubwa kusafishwa kwenye hospitali za binafsi na huku ni huduma ambayo wangepewa hospitali za serikali kama mgonjwa mwingine yeyote na kama una bima hulipi chochote.

Nachochea utoaji mimba?? I dont know... i dont support abotion but sitaki mtu afe au apate shida baada ya kutoa mimba kitu ambacho kinazuilika

Back to the topic...

Mwanamke baada ya mimba kutoka huwa anaweza kurudi kwenye mzunguko wake wa kawaida maana yake yai kutoka baada ya siku 14 hivyo sio lazima uone siku zako kwanza ndio useme upo katika hatari ya kupata ujauzito... kwa sababu yai linatoka kwanza ndio hedhi baadae inatoka.. hivyo unaweza kupata mimba na huku bado hujaona siku zako..ndio maana nilikuwa nasisitiza kutymia uzazi wa mpango au kuacha kufanya mapenzi kabla ya angalau wiki 6 miezi mitatu mpaka 6 ndio upate ujauzito

Be healthy and happy
 I love medicine  i love humanity
@ dr.ibu
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

Nini cha kufanya mimba ikitoka??

NINI CHA KUFANYA MIMBA IKITOKA AU BAADA YA KUTOA MIMBA..

Baada ya mimba kutoka au mimba ikitoka kutokana na sababu mbalimbali iwe umekunywa dawa bila kujua au kwa kujua zikasababisha mimba kutoka basi kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa kuzingatia...kwanza kama ndio umeona damu tu imetoka nenda hospitali  mara moja kwa sababu damu ikitoka sana inasababisha upungufu wa damu na moyo huwa unaweza kufeli... pia unatakiwa kuhakikisha hakuna mabaki ya kiumbe au masalia ya damu yanayobaki kwenye mfuko wa uzazi na njia pekee ni kwenda hospitali kusafishwa kizazi.. lakini pia unatakiwa kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya bacteria.. hii ni kutokana na kwamba mlango wa shingo ya kizazi upo wazi baada ya mimba kutoka hivyo inakuwa kwenye hatari ya kupata infection....ko unapata antibiotics angalau siku 7 mpaka 10.... tatu ni kutafuta chanzo cha mimba kutoka kama mimba imetoka inaweza sababu iliyosababisha mimba moja kutoka ikasababisha mimba inayofuata pia ikatoka... hivyo ni vizuri kutafuta chanzo ili kutibiwa kabla ya kupata mimba nyingine..
Nne ni uzazi wa mpango..
Ni rahisi zaidi mtu kupata mimba baada ya mimba kutoka pindi tu atakapofanya mapenzi...
Hivyo sio lazima aanze kupata mzunguko wake ndio awe katika hatari ya kupata ujauzito. Hatari yake ni kuwa chanzo chake cha mimba kutoka kinaweza kusababisha mimba kutoka tena na pia via vyake vya uzazi vinakuwa havijatengamaa kupata nguvu ya kubeba mimba tena kitu ambacho ni hatari kwa mama na mtoto aliyepo tumboni... hivyo tunashauri mama asijihusishe na kufanya mapenzi baada ya mimba kutoka au kuzaa mpaka siku 42 zitimie wiki 6 au mwezi mmoja na wiki mbili... lakini tunashauri aipate mimba mpaka angalau miezi mitatu mpaka sita baada ya kupoteza mimba...

Nini madhara ya kufanya mapenzi mapema mara tu baada ya mimba kutoka au kuzaa.?
See me at www.ibumd.blogspot.com kwa muendelezo
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

Mpenzi wangu ana ugonjwa wa sickle cell anatumia dawa naombeni ushauri

Topic.For istance ulikuwa na mpenz na mnapendana saana toka upo fom four ye akiwa fom two, mkaishi vizuri   kwa upendo na kwa ahati kuwa mtakuja kuoana.

Mkakua wew ukapanda advanc asichana akamaliza fom four lenu bado ni moja, msichana anaheshima sana, anawaheshimu ndg zako alafu mcha mungu.

Baada ya kumaliza six huku mkiendelea kuwasiliana ukachuguliwa chuo kikuu nayeye Advance... Baadae ukiwa mwaka wa tatu yeye akanza kusoma chuo mwaka wa kwanza.

Mkaamua awe anakuja kutembea mnaonana maana mmoja Muhimbili mwingine Udsm lakin baadae akija akawa anameza dawa za kuongeza dam baada ya kumuhoji vizur akasema anatatizo la dam tuu.
Ukaanza kufuatilia kwa rafik zake ukaja kuambia hua anaishiwa dam mara kwa mara na kuishiwa nguvu Yan kumbe ana sikle cell

Utachukua uamuz gan yeye anasikle cell isiyo na dalili za nje utamuacha au?? NAOMBEN USHAURI

Ushauri : kabla ya kukupa ushauri yafaa ukaujua ugonjwa kwanza ili ikusaidie kuamua na ndio jukumu langu kama daktari.Okey actually sickle cell ni seli mundu kwa kiswahili.. ni hali tu ambayo umbo la seli hai nyekundu  za damu linakuwa kama mwezi mchanga au mundu au sickle ile ya kukatia majani ya ng'ombe ndio jina lilikotoka... seli hai nyekundu za damu ndio seli zinazohusiana na kusafirisha hewa ndani ya mwili wa binadamu. Kawaida huwa zinakuwa na umbo la duara liliobonyea katikati kama disc. Ambapo watu wenye sickle cell wanakuwa na tofauti hiyo. Huu ni ugonjwa  wa kurithi ambao lazima urithi kwa wazazi wote wawili baba na mama. Baba na mama wanaweza wakawa na vinasaba  vya sickle cell lakini hawana ugonjwa AS(heterozygous )  lakini wana hatari ya kuzaa mtoto mwenye sickle SS cell kwa uwezekano wa 25?  Ila kama mmoja wa wazazi ana ugonjwa wa sickle cell SS na baba yuko kawaida hana hata vinasaba AA watazaa watoto wenye vinasaba lakini hawana ugonjwa wa sickle cell AS. Kumbukumbu ya genetics kidogo...
Watu wenye sickle cell wanaishi kama watu wengine tu na wengine hugundulika ukubwani hadi miaka ya 40?
Matatizo wanayopata watu wenye sickle cell..
Mara nyingi matatizo wanayopata yanatokana na ile shape ya hizo seli hai nyekundu...
Kwa seli zilivyo haziwezi kudumu muda mrefu kama  seli hai nyekundu za kawaida... seli hai nyekundu zinaishi siku 120 lakini zenye sickle cell zinaishi siku hadi 15 tu. Hivyo mtu huyu atakuwa na upungufu wa damu wa kudumu. Mtu wa kawaida damu yake hb ni 11 hadi 17 lakini kwa hawa watu wanakuwa na damu mpaka 6 au 7 na huwa hazifanani wengine 8, 9 ,10 na wengine kawaida..kwa hiyo huwa tunawapa dawa za kuongeza damu kila siku kidonge kimoja cha folic acid.
Itaendelea
Dr.ibu 
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

Swali:Nimetumia dawa za uzazi wa mpango damu inatoka haikatiki nini shida?

 Mgonjwa: Habari za uxubuhi my dr mwanamke ametumia dawa za family plan bt tangu achome damu haikatiki nn solution ya hapo
 Dr.ibu: Dawa za family planing zipo za njia tofauti... vidonge, za kuchoma, vipandikizi na loop au kitanzi,  n.k ... katika pia zipo njia za kutumia za kutumia kila tendo mf.condom zipo za kutumia kila siku mf.vidonge zipo za baada ya muda fulani... mf. Za kuchoma kila baada ya miezi mitatu, kipandikizi kila baada ya miaka mitano na loop kila baada ya miaka mitano na nyingine miaka 10... na emergency kama p2 na p1
Uzazi wa mpango ni bure..

Madhara yake zilizonyingi zinaleta kitu tunaita unscheduled bleeding yaani unatoa damu bila ratiba maalum... hali hiyo huwa inatokana na ile hali ya hormone ulizoingiza kupitia zile dawa ulizotumia... mara nyingi huwatokea watu ambao ni mara ya kwanza kutumia na pia hutokea siku za mwanzo baada ya kutumia njia fulani ya uzazi wa mpango... utokaji huu wa damu hupungua jinsi siku zinavyozidi kwenda na baadae huacha kabisa.. tafiti zinaonesha karibia utokaji damu unaotokana na njia zote za uzazi wa mpango unapungua au kutibiwa na hormone ya estrogen.. kwahiyo ukipewa estrogen hormon zote zinakaa sawa mwilini na hivyo damu inaacha kutoka.
Sasa kuna dawa gani yenye estrogen... hii ni homoni ambayo wataalamu wameiweka kwenye vidonge na wanatumia trade name au majina ya bidhaa mbalimbali  lakini ukienda pharmacy mwambie unaomba estradiol itakusaidia

Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

Nina ujauzito na tumbo linauma chini ya kitovu..

Swali.Nina ujauzito wa mwez mmoj na nusu lakn tumb linauma afu nakosa hamu ya kula
JIBu: Leo naomba tuelewane ujauzito huleta upungufu kidogo wa kinga mwilini ili mtoto aweze kukaa tumboni kwa sababu la sivyo kinga ya mwili itaua mtoto... kwa sababu mtoto aliyepo tumboni huwa anakuwa kama kitu au kiumbe kigeni ambacho hakikutakiwa kuwepo.. hivyo kinga ya mwili inapopungua unakuwa katika hatari ya kupata magonjwa tofauti na mtu wa kawaida.. na ukipata ugonjwa utakuwa wa nguvu zaidi na dalili zake zinakuwa kali zaidi kuliko ambaye hana ujauzito... magonjwa ambayo yanawashambulia sana ni UTI na malaria.. ndio maana tunashauri utumie dawa za malaria Sp na ulale kwenye NET kila siku.. lakini kwako nadhani utakuwa na UTI ambayo dalili zake ni..

1. Kuumwa tumbo hasa chini ya kitovu
2.homa na mwili kuchoka
3.kichwa kuuma na wakati mwingine kukosa hamu ya kula
4.maumivu unapokojoa
5.kukojoa mara kwa mara


Kwa mjamzito inatia changamoto kwa  sababu anakojoa mara kwa mara kawaida kwa sababu ni mjamzito lakini pia akikosa hamu ya kula,homa, na kichwa kuuma inaweza kuwa malaria na kwa sababu hajaanza dozi ya dawa za kuzuia malaria.
 Kujua ni kutumia kipimo kupima malaria na UTI kujua nani anakusumbua japo kwa sababu tumbo linauma more likely utakuwa na UTI maabukizi kwenye njia ya mkojo.

Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 0767357271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy

Saturday, 6 October 2018

KANSA YA MATITI

Wiki ya kansa ya matiti duniani...

Kansa ya matiti ni kati ya kansa au saratani ambazo zipo juu katika kuathiri afya ya wanawake duniani..kwa Tanzania ni ya pili ikitanguliwa na kansa ya shingo ya kizazi.

Hii huanza kama uvimbe ambao huwa hauonekani bali mtu anaweza kuuhisi akiwa anaoga au kujigusa au wakati mwingine mtu mwingine anaweza kuuhisi akiwa anagusa titi lake..
Hukua haraka na huweza kusababisha titi kuvimba, kubadilika rangi, baadae ngozi yake kuwa kama ganda la chungwa..lakini pia huweza kutokea kidonda ambacho hakina maumivu au unaweza kushangaa titi halichezi linakuwa linashikana  na kifua hata ukiinama halichezi... baadae mtu huweza kuwa na mitoki ikiwa kwapani ikivimba au kuwa na vidonda.. baadae kansa hii huweza kusambaa sehemu mbalimbali mwilini ikiwepo mifupa hasa ya mgongoni mtu anakuwa na maumivu ya mgongo na kiuno na wakati mwingine kuvunjika hata akidondoka kidogo tu.. kwenye ubongo ambapo mtu huwa anaweza kuwa kama na kifafa, kichwa kuuma sana hasa asubuhi na pengine kupoteza fahamu na kupoteza kumbukumbu...kwenye mapafu anakuwa anashindwa kupumua vizuri, kokohoa damu, na kifua kubana au kuuma... pia tumbo linaweza kujaa maji na kuvimba sana..

Saratani hii kama kansa nyingine chanzo hasa hakijulikani isipokuwa kuna vihatarishi ambavyo mtu akiwa navyo basi anaweza kuwa kwenye hatari ya kupata kansa ya matiti

1.sigara na pombe
2.uzito mkubwa
3.kama mtu kwenye familia aliwahi kuwa ugonjwa huu..wengine pia wanakuwa kwenye hatari... na kama alikuwa na kansa kwenye matiti yote mawili hatari inaongezeka pia kama aliipata akiwa na umri wa chini ya miaka 50 hatari inakuwa kubwa zaidi
4.utoaji wa mimba.. pia mimba inavozidi kuwa na miezi mingi ikitolewa au ikitoka hatari inazidi kuongezeka
5.kama ulishawahi kupata kansa hii unakuwa katika hatari ya kupata tena mara ya pili hata ukipona.
6.kuwa na uvimbe wowote kwenye ziwa kunakuweka katika hatari ya kupata kansa ya ziwa
7.kutokuwa na mtoto mpaka miaka 35 ndio maana zamani ulikuwa unajulikana kama ugonjwa wa masister
8.kuvunja ungo mapema kabla ya miaka 12
9.kuwa na watoto wachache kama mmoja pia ni hatari
10.kutumia dawa za homoni kwa wazee

NINI CHA KUFANYA
1.kagua matiti yako mara kwa mara unapooga
2.acha uvutaji wa sigara pia usikae na wavuta sigara,punguza uzito kwa kufanya mazoezi na punguza unywaji wa pombe
3.kama una ndugu alishawahi kuwa na ugonjwa huu fanya kipimo mamogram mara kwa mara angalau mara moja kwa miezi sita mpaka mwaka mmoja
4.ukihisi uvimbe ambao sio wa kawaida uwahi hospital haraka ukachunguzwe zaidi kumbuka inatibika ukiwahi.

Itaendelea
@dr.ibu
Acha maoni ako hapo chini pia unaweza kutuma swali lako kupitia whatsap no 076757271 jina lako litakua siri kujiunga na group la whatsap bonyeza hapo https://chat.whatsapp.com/3fsRnLDkTZIFMqasAjJXWU Be healthy and happy