Monday, 17 September 2018

Mdogo wangu alitoboa masikio na sindano masikio yametoka uvimbe je dawa yake ni nin?

 JIBU
 la sikio kwanza nakushauri asitibu kienyeji sana aende hospital Kutibu hapo inategemeana na ukubwa wa uvimbe... kama ni mdogo sana atapewa antibiotics na za maumivu tu atapona kama ni mkubwa atapasuliwa utakamuliwa atapewa dawa za maumivu na antibiotics

 Lakini tujifunze nini imetokea kwenye sikio lake.....kwenye ngozi kuna wadudu wengi sana ikiwemo bacteria.... bacteria maarufu zaidi anayeishi kwenye ngozi ni staphylococcus aureus anaishi bila kusababisha shida yoyote kama (normal flora)mpaka akiingia kwenye sehemu nyingine ya mwili ndio husababisha shida huyu ndio husababisha majipu na miwasho na vipele vingi kwenye ngozi... sasa mtu ukijitoboa ngozi au kwa hapo kutoga masikio bila kusafisha lile eneo kwa dawa au spirit unampa uwezo wa kuingia kwenye sehemu ya ndani anayoweza kuleta madhara...ndio maana kabla ya upasuaji huwa tunasafisha ngozi yote kwa iodine ili kuua kwanza hawa wadudu.... na tunaosha mikono kwa dawa maalumu pamoja na kuvaa gloves maalumu kuzuia wadudu hawa wasilete madhara lakini pia tunaongeza na antibiotics za kutumia ili hata kama wameingia wafe na ile dawa

2 comments:

Anonymous said...

Mtaalamu wa mitishamba toka tanga dr karimu anatibu matatizo ya masikio kuunguruma uziwi @ kuondoa harufu mbaya na maji ukeni @ kuondoa kitambi @@ kukuza uume na kutibu UTI sugu & magonjwa ya uzazi wasiliana nae
0676039091

Anonymous said...

Dokta nina shida ya uo.uvimbe sikion.nashida na namba yako